• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serena Williams atarajiwa kumkaribisha mtoto wake kwanza Septemba

  (GMT+08:00) 2017-04-20 09:11:14

  Serena Williams anatarajiwa kupata mwenziwe mpya katika tenisi kwani hivi sasa amekuwa mjamzito kwa mara ya kwanza. Mchezaji huyo aliposti picha kwenye Snapchat Jumatano akidokeza kuwa ana ujauzito wa wiki 20. Picha hiyo aliyotuma haikudumu sana baada ya kuifuta na kuacha mswali mengi kama kweli ni mjamzito au la. Hata hivyo, afisa mahusiano wake Kelly Bush Novak ameithibitishia ESPN kwamba nyota huyo wa tenisi kweli ni mjauzito na anatarajia kujifungua kwenye mwezi wa tisa.

  Serena anashikilia rikodi ya kushinda mataji mengi ya Grand Slam kuliko mchezaji mwingine yeyote katika mashindano ya wazi. Mwezi January, alitwaa taji lake la 23 kwenye michuano ya wazi ya Australia baada ya kumshinda mdogo wake Venus. Na mwezi Machi, alijitoa kwenye michuano ya wazi ya BNP Paribas baada ya kuumia goti. Hadi sasa hajatangaza ana mpango gani kwenye mashindano ya tenis.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako