• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Safari ya Leicester City katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya yafikia kikomo

  (GMT+08:00) 2017-04-20 09:12:53
  Safari ya Leicester City katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu imefikia kikomo baada ya klabu hiyo ya Uingereza kutoka sare na Atletico Madrid uwanjani King Power.

  Leicester waliondolewa katika hatua ya robo fainali baada ya sare hiyo ya 1-1 kwani kwenye mechi ya mkondo wa kwanza walilazwa 1-0.

  Leicester walitawala mechi hiyo katika uwanja wao wa nyumbani na wakaunda nafasi nyingi za kufunga. Hata hivyo, walijikuta wakiwa na mlima wa kuukwea baada ya Saul Niguez kufunga bao kwa kichwa dakika ya 26.

  Hilo lilimaanisha kwamba walihitaji angalau mabao matatu kipindi cha pili ili kufanikiwa kusonga mbele.

  Jamie Vardy alikomboa bao moja dakika ya 61 lakini Atletico walifanikiwa kujilinda hadi dakika ya mwisho na kuhakikisha wanajiunga na Real Madrid kwenye nusu fainali. Real waliwalaza Bayern Munich ya Ujerumani 4-2 na kupata ushindi wa jumla wa 6-1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako