• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu zilizofanikiwa kuingia nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya zapatikana

  (GMT+08:00) 2017-04-20 09:13:33

  Jana usiku michezo ya pili ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya ilichezwa barani Ulaya, FC Barcelona walikuwa wenyeji wa Juventus ya Italia wakati AS Monaco wakuwa wenyeji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani katika michezo hiyo ya marudiano.

  Barcelona ambao walikuwa wanahitaji ushindi wa kuanzia goli 4-0 ili wasonge mbele dhidi ya Juventus kutokana na mchezo wa kwanza kufungwa kwa magoli 3-0, wamejikuta wakiaga mashindano kwa kulazimishwa sare tasa ya 0-0, huku Dortmund wao wakiodolewa katika hatua hii kwa jumla ya mabao 6-3.

  Dortmund wao mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani walipoteza kwa kukubali kufungwa magoli 3-2, hivyo mchezo wa marudiano walipaswa kupata ushindi walau wa magoli 2-0 ili wasonge mbele, bahati haikuwa kwao na wamejikuta wakiambulia kipigo cha magoli 3-1, ratiba ya nani atacheza na nani itajulikana ijumaa hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako