• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yapinga utaratibu wa TFF kushughulikia suala la pointi 3 ilizopata dhidi ya Kagera

    (GMT+08:00) 2017-04-20 09:14:24
    Klabu ya Simba jana iliibuka na kupinga utaratibu unaotumiwa na TFF katika kushughulikia suala la pointi 3 ilizopewa kutoka klabu ya Kagera Sugar kwa kosa la kumchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi 3, huku ikiituhumu TFF kuwabeba mahasimu wao, Yanga. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema wameshangazwa na kitendo cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kupewa jukumu la kushughulikia maombi ya Kagera Sugar ya kutaka mapitio ya maamuzi ya Kamati ya Saa 72 kwani haina mamlaka hayo kwa mujibu wa utaratibu.

    Manara amesisitiza kuwa lengo la TFF kulipeleka suala hilo kwenye kamati hiyo ni moja ya mbinu za kuhakikisha inaibeba Yanga katika mbio za ubingwa, na kwamba utendaji kazi wa kamati hiyo siku zote umekuwa si wa haki kwa upande wa Simba. Pamoja na hayo yote amemuomba Rais Magufuli kuingilia kati jambo hilo kwa kuwa mpira wa miguu umebeba dhamana kubwa kwenye mioyo ya watu pia kuwa na nguvu kubwa kuliko siasa kabla hawajaamua kufanya maamuzi mengine kutokana na kile wanachokiita kuwa ni hujuma wanayofanyiwa na TFF.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako