• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Arsene Weger aanza tambo baada ya kuishinda Middlesbrough 2-1

  (GMT+08:00) 2017-04-20 09:15:05

  Kocha wa Arsenal, Arsene Weger ameibuka na kuanza tambo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Middlesbrough juzi.

  Mabao kutoka kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil yalitosha kuwapa ushindi The Gunners mchezo uliopigwa kwenye dimba la Riverside. Pia kipindi cha pili Alvaro Negredo aliipatia timu yake bao.

  Ushindi huo umewapa nguvu mpya kwenye mbio za kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu ya England inayoelekea ukingoni.

  Timu hiyo imebakiza pointi saba ili kuipiku Manchester City inayoshika nafasi ya nne. Hata hivyo, kikosi hicho cha Guardiola kina michezo zaidi ukilinganisha na Arsenal yenye mchezo mmoja mkononi.

  Kocha huyo raia wa Ufaransa amekiri kwamba awali walianza kupoteza mwelekeo baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka wa Crystal Palace wiki iliyopita.

  Naye kocha wa Middlesbrough Steve Agnew alionekana kuchanganyikiwa kutokana na kupoteza mchezo huo. Hata hivyo alisisitiza kwamba wachezaji wake walipata nafasi na kuonyesha uwezo licha ya kuhitajika kupata point sita ili wajinusuru kushuka daraja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako