• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbwana Samatta anyemelewa na Fenerbahce ya Uturuki

    (GMT+08:00) 2017-04-20 09:18:42

    Habari za usajili barani Ulaya zimeanza kuchukua nafasi wakati huu ambao Ligi Kuu mbalimbali barani humo zinakaribia kumalizika, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameanza kuhusishwa na Fenerbahce ya Uturuki.

    Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji ameanza kuhusishwa na klabu hiyo kutokana na uwezo wake licha ya kuwa maamuzi hayo ya Fenerbahce yanatajwa kushangaza wengi. Fenerbahce kwa sasa wanatafuta mbadala wa mshambuliaji wao Robin van Persie ambaye anaonekana kuchoka.

    Samatta ambaye ana umri wa miaka 24 anatajwa kutazamiwa na Fenerbahce kumrithi Robin van Persie aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal na ManUnited yza Uingereza. Wachezaji wengine wanaotazamiwa na Thomas Bruns, Theo Bongoda na Ridgeciano Haps.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako