• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano na waandishi wa habari wa Tamasha ya Filamu ya Nchi za BRICS ya mwaka 2017 wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2017-04-20 16:29:26

    Mkutano na waandishi wa habari wa Tamasha ya Filamu ya Nchi za BRICS ya mwaka 2017 uliofanyika jana mjini Beijing, umetangaza kwamba tamasha hiyo itafanyika tarehe 23 hadi 27 mwezi Juni mjini Chengdu, kusini magharibi mwa China.

    Filamu inayoitwa "Wakati umeenda wapi?" iliyotengenezwa kwa pamoja na waongozaji watano wa filamu kutoka nchi tano za BRICS, ambao ni Bw Jia Zhangke wa China, Bw Walter Salles wa Brazil, Bw Aleksey Fedorchenko wa Russia, Bw Jahmil X.T. Qubeka wa Afrika Kusini na Bw Madhur Bhandarkar wa India, inatarajiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye ufunguzi wa tamasha hilo.

    Msimamizi mkuu wa filamu hiyo Bw Jia Zhangke amesema filamu hiyo inaweza kuonyesha busara za nchi hizo tano na kuzidisha mawasiliano kati ya watu wa nchi za BRICS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako