• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za China na Iran zafikia makubaliano kuhusu mradi wa kurekebisha kinu cha maji mazito cha Arak

    (GMT+08:00) 2017-04-20 18:54:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amethibitisha kuwa, kampuni za China na Iran zimesaini mswada wa makubaliano ya kwanza kuhusu marekebisho ya kinu cha maji mazito cha Arak, na zitasaini rasmi makubaliano hayo tarehe 23 mwezi huu huko Vienna.

    Marekebisho ya kinu cha maji mazito ni sehemu kuu ya makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyukilia la Iran. Nchi sita za suala la nyukilia la Iran zilianzisha kikundi cha kazi kinachoongozwa na China na Marekani, ambacho kinafanya ushirikiano na Iran kushughulikia mradi wa kurekebisha kinu hicho.

    Bw. Lu Kang amesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kutaweka masharti mazuri ya kuzinduliwa kihalisi kwa mradi wa marekebisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako