• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Benki ya dunia yaonya Kenya dhidi ya kiwango cha deni

  (GMT+08:00) 2017-04-20 19:29:23

  Benki ya dunia imeionya Kenya kwamba kiwango chake cha deni kinaweza kuathiri vibaya uchumi wake.

  Mchumi mkuu wa benki hiyo anayeshughulikia Afrika Albert Zeufack, amesema mikopo ya kufadhili miradi ya miundo mbinu inafaa kufanywa kwa makini ili kupepusha mzozo wa kiuchumi.

  Kenya katika miaka minne iliopita imekopa mabilioni ya fedha kufadhili miradi yake ya miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, kawi na barabara.

  Taakwimu za awali zianaonyesha kwamba deni la Kenya linaweza kupita mapato yake ya kitaifa GDP.

  Mwaka 2016 deni la Kenya lilifikia shilingi trilioni 3.827 sawa na asilimia 51.50 ya pato lake la jumla.

  Shirika la fedha duniani pia limehimiza Kenya kupunguza mwanya wake wa bajeti ili kuweka madeni yake kwenye kiwango inachoweza kusitiri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako