• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kampuni ya China Gezhouba kujenga bwawa la Thwake Kenya

  (GMT+08:00) 2017-04-20 19:29:52

  Wizara ya maji na unyinyizaji nchini Kenya imeipa kandarasi ya shilingi bilioni 36 kampuni ya china kujenga bwawa la Thwake katika kaunti ya Makueni.

  Wizara hiyo imeagiza kandarasi hiyo kupewa China Gezhouba ndani ya siku 14.

  Mamlaka ya ununuzi wa serikali aidha imeondoa kandarasi ya mradi huo iliokuwa imepewa kampuni ya Sinohydro Tianjin pia ya kutoka China.

  Mradi huo utakaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika utasaidia kusambaza maji kwenye mji mpya wa kisasa wa Konza na pia kaunti hiyo ya Makueni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako