• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Karantini ya mifugo yawekwa Uganda kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa midomo na miguu

  (GMT+08:00) 2017-04-20 19:30:20

  Serikali ya Uganda imeweka karantini ya mifugo na biashara ya bidhaa za mifugo katika wilaya Luweero kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa midomo na miguu.

  Kufuatia agizo hilo sasa nyama na maziwa kutoka maeneo hayo hazitaruhusiwa kusafirishwa.

  Tabibu mkuu wa mifugo kwenye wilaya hiyo amesema hadi sasa wamepata matukio zaidi ya 6 ya ugonjwa huo.

  Karantini mpya pia imewekwa katika wilaya ya Nakaseke baada ya ungonjwa huo kuzuka tena.

  Sasa wafugaji wanahofia kuwa wataathirika kwani watategemea mifugo kwa mapato yao .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako