• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Benki ya Dunia yahimiza Tanzania kupunguzia watu umaskini

    (GMT+08:00) 2017-04-20 19:30:59

    Mkurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird amesema mkakati wa Tanzania katika kukuza uchumi, unaweza kusaidia kupunguza idadi ya watu wanaoishi kwenye mstari wa umaskini.

    Amesema kufikia lengo hilo inawezekan, kwa kutumia rasilimali na uwezo wa Tanzania akiongeza kuwa serikali inahitaji kuangalia idadi ya watu ambao wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

    Katika ripoti ya benki hiyo kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania iitwayo 'Fedha iliyo karibu," iliyozinduliwa Aprili 11, imeibainisha kuwa Serikali inapaswa kutengeneza fursa za ajira kwa kujenga uwezo wa sekta binafsi, kuweka sera za kujenga mazingira salama kwa wawekezaji wa biashara kubwa au ndogo.

    Hivi karibuni, kampuni mbalimbali nchini humo zimepunguza wafanyakazi kwa kile kinachoelezwa kuwa, ni kutokana na mdororo wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako