• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wengi watuma maombi ya kufungua viwanda Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-04-20 19:31:18

    Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzaia (TDFA), Hiiti Sillo amesema kuanzia Machi mwaka huu taasisi yake ilimepokea maombi mapya ya usajili wa viwanda 767.

    Amesema katika maombi hayo, viwanda 635 vipya vimesajiliwa kati ya hivyo, 613 vya chakula, kimoja cha dawa na 21 vya vipodozi akisema hiyo ni asilimia 82.8 ya maombi yote jambo linaloashiria kwamba waombaji wengi wanazingatia sheria.

    Amesema katika kipindi hicho TFDA ilifanya tathmini ya maombi 4,762 sawa na asilimia 82.1 ya usajili wa bidhaa za dawa, chakula, vifaatiba na vipodozi, kati ya maombi 5,802 yaliyowasilishwa na 4,322 (75%) yaliidhinishwa na 440 yalikataliwa kwa kutokidhi vigezo vya ubora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako