• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba Abdi Banda huru kucheza mechi sasa

  (GMT+08:00) 2017-04-21 08:56:46

  Beki wa Simba Abdi Banda hivi sasa yupo huru kuitumikia klabu yake ya Simba baada ya jana kutangazwa kumaliza kutumikia adhabu yake. Mchezaji huyo alifungiwa na Bodi ya Ligi baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar, George Kavila

  Kamati ya nidhamu ilikaa juzi na wakati inakaa tayari mchezaji huyo alishakosa mechi mbili hivyo kamati ilipitia na kusikiliza pande zote mbili na kufanya maamuzi kuwa mechi mbili ambazo mchezaji huyo alizikosa ndiyo adhabu yake tosha kwa kosa alilofanya.

  Awali mchezaji huyo baada ya kufanya tukio hilo ambalo mwamuzi hakuliona, alisimamishwa kucheza ligi kuu kusubiri maamuzi, na akakosa michezo dhidi ya Mbao FC na Toto Africans.

  Mchezaji huyo wa Simba ataungana na wachezaji wengine wa klabu hiyo ambao wataingia kambini siku ya Jumapili kujiweka sawa dhidi ya mechi zilizobaki kwenye Ligi Kuu Bara ambazo zinaendelea Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako