• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Man United yaibuka kidedea dhidi ya Anderletch Europa League

  (GMT+08:00) 2017-04-21 08:57:05

  Man United ni miongoni mwa timu zilizocheza mchezo wake wa marudiano wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Anderletch jana usiku katika uwanja wake wa Old Trafford. Man United walicheza mechi hiyo na kukutana na upinzani mkubwa uliopelekea kuongezwa dakika 120.

  Hata hivyo Man United walifanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 2-1 magoli ambayo yalifungwa na Mkhitaryan dakika ya 10 na Marcus Rashford dakika ya 107 wakati goli pekee la Anderletch lilifungwa na Hanni dakika ya 32, hivyo Man United imeingia hatua ya nusu fainali kwa jumla ya magoli ya 3-2.

  Man United wamepata ushindi ulioambatana na pigo kwa mshambuliaji wao tegemeo Zlatan Ibrahimovic kuumia goti la kulia na kutolewa dakika ya 91, hivyo kuumia huko kunatia hofu kubwa kuwa Zlatan anaweza kumaliza msimu huu akiwa nje ya uwanja licha ya kuwa haijathibitika bado.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako