• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda cha magari cha China chaanza kuunda magari na malori nchini Algeria

    (GMT+08:00) 2017-04-21 09:45:49

    Kiwanda cha kutengeneza magari cha China Foton na Kampuni ya uuzaji wa magari ya Algeria KIV wameanzisha mradi wa ubia unaoruhusu kuunda magari madogo na malori nchini Algeria.

    Mradi huo unatarajiwa kuwa na thamani ya dola milioni 5.5 za kimarekani na utatengeneza nafasi 200 za ajira.

    Akiongea baada ya kusainiwa kwa makubaliano kuhusu mradi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya KIV Bw Ahcene Khodja amesema wataanza kuunda magari madogo ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani mbili na nusu, tani tano na tani sita.

    Ikiwa ni sehemu ya juhudi za nchi hiyo kuendeleza viwanda na kupunguza gharama za kuagiza magari, kuanzia mwaka 2014 Algeria iliwataka wauzaji wa magari wageni kuanzisha viwanda vya kuunda magari. Makampuni ya Renault ya Ufaransa na Hyundai ya Korea tayari yanaunda magari nchini humo, wakati kampuni ya Volkswagen ya Ujerumani itaanza mwezi juni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako