• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema iko mbioni kuweka mafunzo ya lugha ya kichina kwenye mtaala wa elimu ya shule za msingi

    (GMT+08:00) 2017-04-21 09:59:14

    Naibu mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya maendeleo ya elimu ya Kenya KICD anayeshughulikia elimu ya msingi Bw. David Njeng'ere amesema, wizara ya elimu ya Kenya inakamilisha taratibu za kuweka mafunzo ya kichina kwenye mtaala wa masomo nchini Kenya.

    Bw. Njeng'ere amesema somo la lugha ya kichina linawekwa kuwa somo la kuchaguliwa katika darasa la nne, na kipaumbele kitakuwa wanafunzi wanaoonesha nia ya kujifunza lugha hiyo.

    Kenya ilitangaza mipango ya kufundisha lugha ya kichina mwaka 2015, chini ya makubaliano ya kuhimiza uhusiano wa elimu na utamaduni kati yake na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako