• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Msumbuji asifu daraja lililojengwa kwa ufadhili wa China

  (GMT+08:00) 2017-04-21 10:13:34

  Rais Filipe Nyusi wa Msumbuji amesifu daraja lililojengwa na kugharamiwa na China katika mto wa Incomati mkoani Maputo, akilitaja daraja hilo kama alama wazi ya maendeleo na kusema linaonesha ahadi ya serikali ya kuboresha maisha ya wananchi.

  Daraja hilo lililogharimu dola milioni 15 za kimarekani limejengwa na Kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China CRBC, ambalo ni sehemu muhimu ya mradi wa barabara za mzunguko za Maputo, ili kurahisisha mawasiliano.

  Daraja hilo lilianza kujengwa mwezi Novemba mwaka jana, na litaunganisha maeneo ya utalii ya Macaneta na Marracuene.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako