• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lailaani Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora

    (GMT+08:00) 2017-04-21 10:14:02
    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeilaani vikali Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya makombora.

    Baraza hilo limeitaka Korea Kaskazini isimamishe mara moja vitendo hivyo vinavyokiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kusema litafuatilia kwa karibu hali ya Korea Kaskazini na kuchukua hatua kali zaidi ikiwemo kuiwekea vikwazo.

    Jeshi la Korea Kusini limesema jumapili Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora katika pwani yake ya mashariki, Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa jaribio hilo halikufanikiwa.

    Taarifa imesema Baraza la Usalama limeeleza wasiwasi mkubwa juu ya Korea Kaskazini kutokana na vitendo vyake ya kuharibu utulivu wa kikanda na hatua zake za uchokozi zinazopuuza maazimio husika yaliyopitishwa kwenye baraza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako