• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika Kusini yasema inazingatia uanachama wake katika kundi la BRICS

  (GMT+08:00) 2017-04-21 16:38:13

  Afrika Kusini inazingatia ahadi yake kwa kundi la BRICS la kuongoza nchi zinazoibuka kiuchumi, na inatarajia kuwa nchi mwanachama inayosaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini humo.

  Akizungumza katika semina iliyofanyika mjini Pretoria, Mkurugenzi mtendaji wa Idara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini Dave Malcomson amesema, BRICS itasaidia mchakato wa kiviwanda nchini humo na bara zima la Afrika kwa kuunga mkono uwezeshaji kwenye sekta za miundombinu na uwekezaji, na kuboresha sekta ya uzalishaji.

  China inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka 2017 wa BRICS utakaofanyika Septemba, ambapo nchi wanachama watajadili ukuaji wa uchumi wa dunia, kuboresha ushirikiano na maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako