• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkurugenzi wa Benki ya Dunia asifu pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja

  (GMT+08:00) 2017-04-21 16:54:13

  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. Jim Yong jana amesema, pendekezo lililotolewa na China kuhusu Ukanda Mmoja na Njia Moja lina umuhimu mkubwa kwa serikali ya China na Benki hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mkutano wa majira ya mchipuko wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, Bw. Jim Yong amesema pendekezo hilo linaonesha jinsi China inavyofuatilia suala la maendeleo ya dunia. Ameongeza kuwa Benki ya Dunia imekuwa ikidumisha uhusiano wa karibu wa ushirikiano na serikali ya China pamoja na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, na uhusiano huo utaimarishwa zaidi katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako