• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Wafanyabiashara wa Marekani watafuta ushirikiano na Rwanda

  (GMT+08:00) 2017-04-21 19:22:52

  Ujumbe wa wafanyabiashara 16 kutoka Marekani wako nchini Rwanda kutafuta ushirikiano na wawekezaji nchini humo.

  Kiongozi wa ujumbe huo Heath Cardie amesema wafanyabiashara wadogo wadogo wanafaa kusaidiwa kifedha kwani wao ndio husukuma mbele uchumi.

  Alisema wafanyabishara hao wa Marekani wangependa kushirikiana na wenzao wa Rwanda kuboresha oparesheni zao za kibiashara na kufungua nafasi zaidi za ajira.

  Zaidi ya wafanyabiashara 300 wa Rwanda wamehudhuria kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na wenzao kutoka Marekekani na kujadili fursa za ushirikiano zilizopo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako