• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mkuu wa Tanzania alitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi kufanya tathmini ya kisayansi

  (GMT+08:00) 2017-04-21 19:23:25

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amelitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lianze kufanya tathmini ya kisayansi kuhusu manufaa ya mifuko yote ya uwekezaji nchini ili kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.

  Amelitaka baraza hilo lifanye tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake. Alitoa agizo hilo juzi wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji katika Uwanja wa Mashujaa

  Alisema mifuko hiyo imesaidia upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na kupunguza kiwango cha umaskini nchini. "Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko hiyo kwa pamoja ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya sh trilioni 1.759 kwa wajasiriamali 400,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako