• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Wakulima Uganda wataka bajeti iongezwe

  (GMT+08:00) 2017-04-21 19:24:09

  Wakulima nchini Uganda wanaitaka serikali kuongeza bajeti ya sekta hiyo kutoka bilioni 823 hadi trilioni moja katika bajeti ya mwaka ujao.

  Wamesema kuongezewa kwa bajeti kutahakikisha kuimarika kwa uzalishaji kwenye sekta hiyo na pia kuboresha oparesheni kwenye taasisi husika za kilimo.

  Wakulima wamesema bajeti ya sasa haitoshi kukidhi matukio ya dharura yanayotishia usalama wa chakula.

  Aliyekuwa waziri wa kilimo nchini humo Samuel Sentumbwe, amesema kwa viwavi jeshi waliovamia mashamba mwezi juni mwaka jana hawangeweza kuthibitiwa kwani serikali ilikosa shiligi bilioni mbili za kukabili dharura hiyo.

  Amesema kama kungekuwa na pesa za kutosha wangethibitiwa nah ivyo kuepusha hasara kubwa ambayo ilifuata baada ya uharibifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako