• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Russia wakutana

    (GMT+08:00) 2017-04-21 19:24:55

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Kazakhstan, amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov huko Astana.

    Mawaziri hao wamebadilishana maoni kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea, na kuahidi kuimarisha mawasiliano, uratibu, kushirikiana katika kusimamia na kudhibiti hali ya peninsula hiyo na kuzuia vitendo vyote vinavyoweza kuongeza mvutano zaidi katika peninsula hiyo.

    Bw. Wang Yi pia amehudhuria Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai uliofanyika nchini Kazakhstan, na kupendekeza wanachama wa jumuiya hiyo kudumisha ushirikiano na kuungana mkono kukabiliana kwa pamoja na changamoto mbalimbali ili kulinda amani na usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako