• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Korea Kaskazini itatekeleza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-04-21 20:21:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, China inasisitiza kuwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea linatelekezwa kwa pande zote na kwa uwiano.

    Bw. Lu Kang amesema China inashikilia kutimiza peninsula ya Korea isiyo ya silaha za nyuklia, kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo, na kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo. Kutokana na hali ya sasa, pande mbalimbali zinapaswa kujizuia na kutofanya vitendo vitakavyozidi kuchochea hali ya wasiwasi ya sehemu hiyo.

    Habari zinasema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeilaani vikali Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya makombora, na limeitaka nchi hiyo isimamishe mara moja vitendo vinavyokiuka maazimio ya Baraza hilo. Pia Baraza hilo limesema litafuatilia kwa karibu hali ya Korea Kaskazini na kuchukua hatua kali zaidi ikiwemo kuiwekea vikwazo.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako