• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yaisaidia Ethiopia kuongeza uzalishaji wa saruji

    (GMT+08:00) 2017-04-21 20:22:30

    Kiwanda cha saruji ya Ethiopia kilichojengwa na kampuni ya China NHI kimezinduliwa, kwa sherehe iliyohudhuriwa na Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Hailemariam, aliyesifu mchango unaotolewa na China katika kuongeza uzalishaji wa saruji nchini Ethiopia.

    Amesema uzinduzi wa kiwanda hicho utaongeza uzalishaji wa saruji nchini Ethiopia kufikia tani milioni 16.4 kwa mwaka, mara kumi ya kiasi cha miaka 10 iliyopita.

    Mkuu wa kampuni iliyojenga kiwanda hicho Bw. Liu Hequn amesema kwamba kiwanda hicho kina maana kubwa kiuchumi na kijamii, na kinaonyesha urafiki wa dhati kati ya China na Afrika.

    Kitakapoanza kazi, kiwanda hicho kitaweza kuzalisha tani 4,500 za saruji kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako