• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kuvutia uwekezaji kutoka China

    (GMT+08:00) 2017-04-22 17:32:46

    Balozi wa Uganda nchini China Charles Madibo Wagidoso amesema Uganda inapenda kuvutia zaidi uwekezaji toka China kwa sera nzuri zaidi za uwekezaji ikiwemo msamaha wa kodi, kuharakisha mchakato wa uchunguzi wa uwekezaji na uhuru wa kuhamisha mitaji ndani na nje ya Uganda.

    Balozi Wagidoso ameyasema hayo alipohudhuria mkutano wa kukuza uwekezaji katika mji wa Fuzhou, mji mkuu wa jimbo la mashariki ya China Fujian.

    Wagidoso amewahakikishia wawekezaji toka China kuwa maslahi yao yatalindwa, na kuwakaribisha wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo. Vilevile ametoa mfano wa makapuni ya China, Guangdong na Dongsong kuwa na mafanikio nchini humo kwa kuzalisha mbolea ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa kilimo na imeweza kutoa ajira 3,000 na kuzalisha kodi ya mapato kwa serikali za mitaa.

    China inashika nafasi ya kwanza katika suala la uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini Uganda, ambao thamani yake imefikia jumla ya dola za kimarekani bilioni 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako