• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chombo cha kupeleka mizigo angani cha China chafanikiwa kuungana na maabara ya anga ya juu

  (GMT+08:00) 2017-04-22 17:34:10

  Chombo cha kupeleka mizigo kwenye anga ya juu cha China Tianzhou-1 kimeungana na maabara ya anga ya juu Tiangong-2 kwa mafanikio saa sita na dakika 23 leo mchana.

  Hii ni mara ya kwanza kwa vyombo hivi vilivyosanifiwa na China kwa kujitegemea kuungana kwa pamoja.

  Chombo cha kupeleka mizigo cha Tianzhou-1 kikidhibitiwa na wanasayansi wa China, kilibadilisha njia kwa mara kadhaa angani, na kuingia katika hali ya kujidhibiti yenyewe saa nne na dakika 2 leo asubuhi, na kukaribia maabara ya Tiangong-2 hatua kwa hatua. Saa sita na dakika 16, vipuri vya kuunganisha vyombo viwili viligusana, na baada ya kufanya hatua mbalimbali kwa mujibu wa mpango, vyombo hivi viwili vilifanikiwa kuungana pamoja.

  Baadaye vyombo hivi viwili vitafanya kazi ya kujaza nishati njiani, na kufanya majaribio mbalimbali ya safari ya anga ya juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako