• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wataka kuwepo sera za kuboresha sayansi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-04-23 16:48:42

    Wanasayansi wa teknolojia ya bailojia nchini Kenya wameitaka serikali kutunga sera mpya zitakazoboresha kazi za sayansi nchini humo.

    Afisa Mipango wa Baraza la Wadau wa Teknolojia ya Bailojia la Afrika Kennedy Oyugi amesema kuwa utafiti wa kisayansi unapaswa kuungwa mkono zaidi kuliko kukatishwa tamaa na watunga sera. Amefafanua kuwa sera zitakazoweka kipaumbele kutoa pesa na kuunga mkono sayansi zinapaswa kuangaliwa zaidi. Aidha amesema suluhu zilizopo za kisayansi juu ya mahitaji ya lazima kama vile ukame na wadudu mashambani zinapaswa kuruhuisiwa kufanyiwa majaribio kitaifa na mamlaka za nchi.

    Amesisitiza kuwa sayansi ni sehemu muhimu ya maisha kwasababu inaunganisha watu wa sekta zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako