• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa fedha wa G20 wafikia makubaliano kuhusu biashara huria na masoko ya wazi

    (GMT+08:00) 2017-04-23 17:25:03

    Mawaziri wa fedha kutoka kundi la nchi 20 zinazoongoza kwa uchumi duniani G20 wamekubaliana kwa mapana kuwa biashara huria na masoko ya wazi ni muhimu katika kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia.

    Waziri wa fedha wa Ujerumani, nchi mwenyekiti wa kundi hilo kwa mwaka huu Wolfgang Schaeuble alisema baada ya kukamilika kwa mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu za G20 uliofanyika mjini Washington, sera ya kujilinda inaweza kuathiri uchumi wa dunia na makundi ya kiuchumi kwa pamoja. Naye mkuu wa benki kuu ya Ujerumani Jens Weidmann amesema karibu kila mtu amesisitiza umuhimu wa kufungua masoko kwa nje badala ya kuongeza vizuizi vya kibiashara kwenye mkutano huo.

    Wakati huohuo, waziri wa fedha wa China Xiao Jie amesema nchi mbalimbali za kundi la G20 zinapaswa kuratibu sera zao za uchumi wa jumla, kuimarisha mageuzi ya kimuundo, kuhimiza maendeleo ya uchumi wa wazi wa dunia, na kwamba China ina imani ya kutimiza lengo lililowekwa la asilimia 6.5 ya ukuaji wa uchumi wake na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako