• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini haina nia ya kuanzisha tena mazungumzo na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-04-23 18:28:03

    Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema nchi hiyo haina nia yoyote ya kuanzisha tena mazungumzo na Marekani kama Marekani inakataa kuacha sera za kiadui dhidi yake.

    Limesema Marekani inaitupia lawama Korea Kaskazini kwa kushindwa kwa mazungumzo kati ya nchi hizo, ili kutetea sera za kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuishinikiza kijeshi Korea Kaskazini. Pia limesema Marekani imeeleza kuwa haitarajii kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini, na inapanga kufanya operesheni za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, kuizuia nchi hiyo kuendeleza uwezo wa kujilinda, kuendelea kuishinikiza kijeshi na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, pamoja na kuweka silaha za nyuklia nchini Korea Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako