• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda asema sekta ya viwanda na umeme ni muhimu katika kulinda rasilimali ya ardhi

    (GMT+08:00) 2017-04-23 18:47:50

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema sekta ya viwanda na umeme ni muhimu katika kulinda rasilimali ya ardhi ya bara la Afrika.

    Akiongea kwenye kongamano la 6 la Tana kuhusu usalama wa Afrika ambalo linafanyika kwa siku mbili mjini Bahir Dar nchini Ethiopia, rais Museveni amesisitiza umuhimu wa kuelimisha watu pamoja na maendeleo ya miundo mbinu. Amesema kama nchi haiendelei itakuwa ama haiwezi kutumia rasilimali zake au kuangukia kwenye mikono ya makampuni ya nje yasio na uaminifu. Hata hivyo amewataka waafrika kuchukua juhudi kulingana na hali zao maalumu na kuangalia kwa ndani suluhu ya matatizo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako