• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yapokonywa pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar

    (GMT+08:00) 2017-04-24 09:02:35
    Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuipokonya Simba pointi tatu na mabao matatu ambazo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar. Wiki mbili zilizopita, Simba SC ilipoteza mchezo huo dhidi ya Kagera kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera katika Ligi Kuu ya Bara lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga Kagera kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano, ndipo ikapewa ushindi huo kupitia Kamati ya Saa 72.

    Mara baada ya kamati hiyo kuipa Simba pointi Kagera ikaomba kupitiwa upya kwa suala hilo na ndipo TFF ikatangaza kuwa suala hilo sasa litakuwa chini ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo imetoa maamuzi hayo.

    Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa kuna sababu kadhaa zilizochangia kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ambapo alizitaja kuwa ni malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati muafaka tangu mchezo ulipochezwa, malalamiko yao hayakuwa katika njia ya maandishi, rufaa ya Simba haikulipiwa ada, kikao cha Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali kutokana na kuwashirikisha watu ambao hawana uhalali wa kuwa kwenye kikao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako