• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yatinga fainali kombe la FA baada ya kuichapa Manchester City mabao 2-1

    (GMT+08:00) 2017-04-24 09:03:22
    Washika mitutu wa London klabu ya Arsenal imetinga fainali ya kombe la FA baada ya kuwachapa Manchester City kwa mabao 2-1 .

    Mchezo huo wa nusu fainali ulichukua dakika 120 baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 katika dakika tisini za muda wa kawaida.

    Man City ndio walioanza kuzifumania nyavu za Arsenal kwa goli la dakika ya 62 liliowekwa kambani na mshambuliaji wake mahiri Sergio Aguero Kun.

    Beki wa kushoto wa Arsenal Nacho Monreal alisawazisha bao lilo katika dakika ya 71 ya mchezo .

    Alexis Sanchez aliipeleka timu yake fainali kwa goli alilofunga katika dakika ya 101, kufuatia patashika ya mpira wa kutengwa iliyotokea kwenye goli la City.

    Fainali ya mchezo wa kombe la FA itapigwa Mei 27 katika dimba la Wembley ambapo Arsena watakipiga na Chelsea kuwania ubingwa wa kikombe hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako