• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala cha Afrika Kusini chapendekeza mabadiliko ya kimuundo, na kuhimiza nidhamu

    (GMT+08:00) 2017-04-24 09:12:25

    Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimependekeza mabadiliko ya kimuundo yenye lengo la kufanya utendaji wake uwe na ufanisi.

    Akiongea na waandishi wa habari mjini Johannesburg, mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya ANC Bw Fikile Mbalula amesema chama cha ANC kinapenda kuwachagua viongozi wenye uwezo na wenye nidhamu, waliopewa mafunzo ya kuhudumia umma.

    Kwenye mkutano wa taifa kuhusu sera unaotarajiwa kufanyika kati ya juni 30 na Julai 5, baadhi ya mapendekezo yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na kutuma makada wake kwenye mafunzo nchini China, kupunguza idadi ya wajumbe wa kamati kuu yenye wajumbe 86, na kuanzisha idara za chama kwenye sekta mbalimbali za jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako