Waziri Wang Yi amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari baada ya kukutana na mwenzake wa Ugiriki huko Athens. Alisema China siku zote inashikilia msimamo thabiti wa kuunga mkono kuondoa silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea na kulinda amani na utulivu kwa njia ya amani. Amesema ingawa China si kiini cha mgongano huo, imeendelea na juhudi za kurudisha mazungumzo ya amani kati ya pande husika, na hivi karibuni imetoa pendekezo la ufumbuzi linaloungwa mkono na nchi nyingi. Bw. Wang ameongeza kuwa China pia inazikaribisha nchi nyingine kutoa suluhisho lao, zikiwa na nia ya dhati ya kulitatua suala hilo kwa amani.
Bw. Wang Yi pia amesema China itaendelea kutekeleza majukumu yake na kutoa mchango wa kiujenzi katika kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |