• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw Macron na Bibi Le Pen waingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa

  (GMT+08:00) 2017-04-24 09:53:12

  Kwa mujibu wa makadirio ya upigaji kura na matokeo ya mwanzo ya kiserikali, mgombea wa chama cha mrengo wa kati Bw. Emmanuel Macron aliyekuwa waziri wa uchumi, na mgombea wa chama cha mrengo wa kulia Bibi Marine Le Pen wameongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa.

  Makadirio mapya yaliyotolewa na kampuni ya utafiti ya Elabe kupitia televisheni ya BFMTV yameonesha kuwa Bw Macron ameongoza kwa kupata asilimia 24 ya kura zote, akifuatiwa na Bibi Le Pen aliyepata asilimia 21.8 ya kura.

  Jumla ya wagombea 11 walishiriki kwenye uchaguzi wa urais wa Ufaransa, na wagombea hao wawili wanaoongoza wataingia katika duru ya pili itakayofanyika Mei 7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako