• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yahimiza uwekezaji mkubwa katika usalama wa mtandao wa Internet

    (GMT+08:00) 2017-04-24 09:53:33

    Kenya imetoa wito kuongeza uwekezaji katika usalama wa mtandao wa Internet ili kuzuia matukio yanayoongezeka ya uhalifu kupitia mtandao Internet unaolenga uchumi wa kidigitali wa nchi hiyo.

    Waziri wa teknolojia ya mawasiliano ya habari wa Kenya Bw. Joe Mucheru amehimiza sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya usalama wa mtandao wa Internet, ili kusaidia juhudi za serikali kuzuia uhalifu.

    Katika mkutano wa baraza la kuboresha miundombinu ya shule, Bw. Mucheru amesema wamewasilisha mswada wa sheria ya kompyuta na uhalifu wa mtandao mwaka 2016 bungeni. Wanataka sheria hiyo itoe adhabu kali zaidi kwa uhalifu wa mtandao na ujasusi kupitia mtandao wa Internet.

    Kenya iko miongoni mwa nchi za Afrika zinazokabiliwa na hatari kubwa ya kushambuliwa kupitia mtandao wa Internet, kutokana na matumizi makubwa ya mtandao wa Internet katika pande zote za maisha nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako