• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria yamwita balozi wa Morocco kuhusu suala la wakimbizi wa Syria

    (GMT+08:00) 2017-04-24 10:23:35
    Wizara ya mambo ya nje ya Algeria imemwita balozi wa Morocco ikipinga madai ya Morocco kuhusu Algeria kuwafukuzia wakimbizi wa Syria nchini Morocco.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Algeria imesema Algeria inapinga vikali madai ya Morroco kuilaani Algeria kuwafukuzia Morocco wakimbizi wa Syira kupitia mipaka ya nchi hiyo mbili.

    Taarifa imeongeza kuwa madai hayo yasiyo na msingi wowote yanalenga kuharibu kiwango cha maadili cha Algeria na desturi zake za ukarimu kwa wageni.

    Vyombo vya habari vya Morocco vimeripoti kwamba wakimbizi 55 wa Syria kutoka Algeria wamekumbwa na matatizo mipakani, Morocco imewazuia kuingia na kuishutumu Algeria kwa kuwafukuzia Morroco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako