Kiongozi wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini masuala ya haki za binadamu Bw Eugene Nindorera amesema hakuna yeyote aliyekamatwa au kutiwa mbaroni kwa kuhusika na hatia ya mauaji mjini Wau.
Vurugu zilizotokea mjini Wau mwezi Aprili zimesababisha vifo vya askari 19 wa jeshi la Sudan Kusini SPLA, na wananchi wengine wasiopungua 28. Serikali ya jimbo la Wau imeanzisha kamati kwa ajili ya kuandaa ripoti ya uchunguzi ili kuwatambua wahusika wa vurugu na kuwafikisha mbele ya sheria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |