• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 37 wa kundi la IS wauawa nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-04-24 17:06:25
    Wapiganaji 37 wa kundi la IS wameuawa katika operesheni ya kijeshi inayoendelea kwenye mkoa wa Nangahar ulioko mashariki mwa Afghanistan.

    Taarifa iliyotolewa na jeshi la Afghanistan imesema, wapiganaji hao wameuawa katika mashambulizi ya anga na ardhini yaliyofanywa na vikosi vya usalama vya Afghanistan katika wilaya ya Achin mkoani Nangarhar katika saa 24 zilizopita.

    Wakati huohuo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inafuatilia kuongezeka kwa mgogoro wa nchini Afghanistan. Geng amesema hayo kutokana na shambulizi lililofanywa na kundi la Taliban dhidi ya kambi ya jeshi la nchi hiyo karibu na mji mkuu wa jimbo la kaskazini la Barh na kusababisha vifo vya watu 140.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako