• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yaapa kuendelea kutengeneza silaha za nyuklia kwa ajili ya kujilinda

    (GMT+08:00) 2017-04-24 19:27:02

    Korea Kaskazini imesema itaendelea kuendeleza silaha za nyuklia kwa ajili ya kujilinda dhidi ya tishio la kijeshi kutoka Marekani.

    Makala iliyochapishwa kwenye gazeti la kila siku la nchini humo Rodong Sinmum imesema, hatua ya Marekani ya kupeleka meli ya kubeba silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea ni ya hatari. Makala hiyo imesema hatua hiyo ni ya usaliti dhidi ya Korea Kaskazini na ni kitendo cha hatari kinachoiweka peninsula hiyo kwenye hali tete zaidi.

    Hivi karibuni Korea Kaskazini imeongeza tuhuma zake kwa Marekani, ikiahidi kujibu kwa kutumia silaha za nyuklia wakati mvutano kwenye peninsula ya Korea ukiongezeka.

    Kuna wasiwasi mkubwa kuwa Korea Kaskazini itafanya jaribio lingine la nyuklia au makombora hapo kesho, ambayo ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa jeshi la wananchi wa Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako