• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Macron aongoza kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu Ufaransa

    (GMT+08:00) 2017-04-25 09:55:26

    Matokeo rasmi yaliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa yamethibitisha kuwa mgombea Bw Emmanuel Macron mwenye mrengo wa kati ameongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini humo.

    Macron amechukua nafasi ya kwanza kuwa kupata asilimia 24.01 ya kura huku nafasi ya pili ikichukuliwa na mpinzani wake Bi Marine Le Pen, kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha National Front, aliyepata asilimia 21.30 ya kura. Watagombea hawa watakutana katika duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika tarehe 7 mwezi ujao.

    Rais Francois Hollande jana amesema atampigia kura Bw Emmanuel Marcon katika duru ya pili ya uchaguzi, kwa kuwa ana uwezo wa kulinda maadili yanayoruhusu umoja wa taifa katika kipindi hiki maalumu. Akihutubia taifa kupitia televisheni, rais Hollande ameonya kuwa msimamo wa kupinga uhamiaji kutoka chama cha mrengo wa kulia utasababisha mgawanyiko mkubwa wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako