• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi na mnadhimu mkuu wa jeshi la Afghanistan wajiuzulu

    (GMT+08:00) 2017-04-25 09:55:46

    Ikulu ya Afghanistan jana imesema waziri wa ulinzi Bw Abdullah Habibi na mnadhimu mkuu wa jeshi la nchi hiyo Jenerali Qadam Shah Shahim wamewasilisha barua za kujiuzulu kwa rais Ashraf Ghani wa Afghanistan, na barua hizo zimepokelewa.

    Vyombo vya habari vya Afghanistan vimesema, viongozi hao wameamua kujiuzulu kutokana na hali mbaya ya usalama nchini humo, hasa tukio la kushambuliwa kwa kambi ya jeshi iliyoko Mazar-i-Sharif, mji mkuu wa mkoa wa Balkh, kaskazini mwa Afghanistan.

    Wakati huo huo, shambulizi la kujitoa mhanga limetokea jana karibu na kituo cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan kilichoko mkoani Khost, ambalo limesababisha vifo vya watu watano na wengine wanane kujeruhiwa.

    Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako