• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani autaka Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-04-25 17:43:30

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema hali ya sasa ya Peninsula ya Korea haikubaliki, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatakiwa kuwa tayari kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vya ziada vyenye nguvu kufuatia majaribio ya nyuklia na makombora ya nchi hiyo.

    Rais Trump amesema hayo jana ikulu alipokutana na mabalozi wa nchi wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Habari nyingine zinasema wajumbe wa mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kutoka Japan, Marekani na Korea Kusini wamefanya majadiliano leo mjini Tokyo. Mjumbe maalum wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani anayeshughulikia masuala ya Korea Kaskazini Bw. Joseph Yun amesema nchi hizo zimekubali kuendelea kushirikiana katika mambo ya diplomasia, jeshi na uchumi.

    Mkurugenzi wa idara ya Asia na Oceania ya wizara ya mambo ya nje ya Japan Bw. Kenji Kanasugi amesema nchi hizo zimefikia maoni ya pamoja kuhusu kuihimiza Korea Kaskazini kujidhibiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako