• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 10 wauawa kwenye shambulizi la bomu kaskazini magharibi mwa Pakistan

    (GMT+08:00) 2017-04-25 18:27:34

    Watu 10 wameuawa na wengine 8 kujeruhiwa baada ya gari moja dogo la abiria kukanyaga bomu lililotegwa ardhini kwenye eneo la kikabila la Kurram Agency, lililo kaskazini magharibi mwa Pakistan.

    Kituo cha televisheni cha Pakistan kimeripoti kuwa watu waliouawa ni pamoja na wanawake na watoto, na kati ya majeruhi kuna wafanyakazi wawili wa sensa ambao walikuwa njiani kufanya sensa ya idadi ya watu kwenye eneo hilo.

    Mpaka sasa hakuna shirika lolote lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Wakati huohuo, jeshi la Pakistan limesema magaidi wakuu wanne waliohusika kufanya uhalifu mkubwa unaohusiana na ugaidi wamenyongwa leo. Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema, magaidi hao walikutwa na hatia ya makosa ya kuua raia wasio na hatia, kuwashambulia askari na taasisi za usalama za Pakistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako