• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 70 wa kundi la PKK wauawa katika shambulizi la anga la Uturuki Syria na Iraq

    (GMT+08:00) 2017-04-26 09:39:17
    Wapiganaji takriban 70 wa Chama cha wafanyakazi cha Kurdistan PKK na tawi lake la YPG wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Uturuki nchini Syria na Iraq.

    Taarifa iliyotolewa na jeshi la Uturuki inasema operesheni hiyo inayolenga kulizuia PKK kufanya magendo ya silaha zinazotumika kufanya mashambulizi nchini Uturuki, imeharibu makazi, ghala la silaha na vituo vya mawasiliano ya kundi hilo.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bw. Mark Toner amesema Uturuki haikuwasiliana na Marekani au nchi nyingine za muungano kabla ya kufanya mashambulizi hayo. Amesema wanasikitishwa kuwa mashambulizi hayo yamesababisha vifo kwa wapiganaji wa Peshmerga, wanaosaidia kupambana na kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako