• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya pamoja ya makubaliano ya suala la nyuklia la Iran yaitisha mkutano wa saba

    (GMT+08:00) 2017-04-26 10:12:37

    Iran na nchi sita za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China na Ujerumani jana zimefanya mkutano wa saba wa tume ya pamoja ya makubaliano ya suala la nyuklia la Iran mjini Vienna, Austria.

    Mwakilishi wa China Bw Dong Zhihua amesema China inaunga mkono makubaliano hayo, ambayo ni matunda ya juhudi za pande zote, na mfano mzuri wa kutatua masuala ya kimataifa kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia. Amesema, pande zote zinatakiwa kuimarisha dhamira ya kisiasa, kutekeleza wajibu kwa makini, na kutatua masuala kwa njia mwafaka, ili kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa kwa ufanisi.

    Ameongeza kwamba China na Iran zimesaini makubaliano ya kwanza ya kibiashara katika kutengeneza upya kituo cha umeme cha nyuklia mjini Arak, ambayo yameonyesha msimamo wa China wa kuwajibika katika kulinda na kutekeleza makubaliano hayo.

    Kwenye mkutano huo, pande zote husika zimebadilishana maoni na kuahidi kudumisha mawasiliano kuhusu utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako