• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto milioni 25 duniani wakosa elimu kutokana na mapambano

    (GMT+08:00) 2017-04-26 18:32:14

    Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, watoto zaidi ya milioni 25 wenye umri kati ya miaka 6 na 15 wanakosa elimu katika nchi 22 zinazoathiriwa na mapambano, ambao wanachukua asilimia 22 ya watoto wote wenye umri huo duniani.

    Taarifa ya UNICEF imesema idadi ya watoto wa kike wanaokosa elimu nchini Sudan Kusini ni asilimia 76, Chad asilimia 53, na Afghanistan asilimia 55.

    UNICEF imesema mfuko unaoitwa "Elimu Haiwezi Kusubiri" ulioanzishwa kwenye mkutano mkuu kuhusu ubinadamu duniani mwezi Mei mwaka jana umekusanya dola za kimarekani milioni 10. Mfuko huo utawapatia elimu bora watoto wanaokimbia makazi yao na wale wanaoishi katika kambi ya wakimbizi nchini Chad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako